
You are most welcome to visit my site. I
hope here you will find the information that you are searching for. Please
be tolerant and patient with me, as this is a bilingual site (English/Swahili).
Sometimes you might encounter an article written both in English and Swahili but
most of the times it will be in one language only.
The site mostly covers
debates, in the written form, that took place in different discussion
forums, which I had with my colleagues. For this reason you will not
only find my very own Swahili-English articles but those of my colleagues as
well.
________________________________
Madhumuni ya kuunda hii site ni
kutokana na ile site ya mawaidha ambayo imeweka kwa makusudi ya kuwadhalilisha
Mashiya, kuwakufurisha Mashiya na kueneza chuki na fitna za Kimadhehebu. Kwa
upande wangu, ikanibidi nichukuwe khatwa ya kujibu tuhma zilizowekwa na muandalizi
wa site ya Mawaidha.
Nitamuomba kwa yule
atakaepitiya site yetu, isije kumpitikiya kuwa kusudio la kuiweka site hiyo ni
kutaka ugomvi baina yetu na Sheikh wa Site ya Mawaidha, kwasababu hiyo sio nia
yetu. Tunachokifanya sisi, ni kujibu zile hoja za Kiwahabbi alizoziweka Sheikh wa
Mawaidha, kwasababu tumeona kuwa ipo haja ya kujibiwa kwa kila tuhma alioiweka.
Tutaona yakuwa lengo na tegemeo la
mwandishi wa hiyo site ya mawaidha ni kutaka kumwaga mbegu za chuki kwa
Wazanzibari kwa kuwafanya Mashiya sio Madhehebu sahih na kuwatoa katika Uislamu.
Jambo hilo siyo geni khasa tukiwasoma wenye itikadi potofu kama akina Ibn Taymiya
wenye fikra kama hizo. Tukiangaliya vizuri tutaona yakuwa muandishi wa hiyo site
ni mmoja wa wafuasi wa Ibn Taymiya ambae kwa sasa wenye kujulikana kwa jina la
Mawahabi!
Tutamuona yakuwa muandishi wa hiyo
site ya mawaidha amejikaza kutaka kupanda hiyo mbegu ya chuki kwa kutumiya
vitabu vya Kishia. Cha kustaajabisha kwa upungufu wake wa elimu hakuweza kutambuwa
yakuwa itikadi za Mashiya siyo kama za kwake, Mashiya hawana hiyo imani yakuwa
vitabu vyao vya hadith ni SAHIH, kama tunavyoona Sahih Bukhari na vyenginevyo.
Tumeweza kuthibitisha mara kwa mara wakati tulipokuwa tukijadiliana nae kwa
kumuona vipi alivyokuwa akihangaika na kutapatapa kwa kuziteteya
hizo hadithi ambazo kwa yoyote yule mwenye kuzisoma kwa uangalifu ataona hadithi
zilizomo ndani ya vitabu vinavyojulikana vitabu vya sahih, haziwezi kuwa ni sahih
zote kama vile Sheikh wa Zanzinet anvyoziweka yeye. Tunatarajia siku za mbele
kudondowa baadhi ya hadithi ziliyomo ndani ya vitabu vinavyoitwa Sahih kwa
kuonesha hadithi ambazo haziwezi kuingiya akilini hata kidogo.
Kwa Mashiya, hawana haja ya
kuhangaika na kusumbuka jawabu yao safi kama hadith haingi akilini basi hutupiliwa
mbali. Huu ndio msimamo wa Mashiya.