Date: Tue, 4 Dec 2001 13:13:06 -0800 (PST)
From: "Mohammed Yusuf" <abulqasimali@yahoo.com>
Subject: Re: [Zanzinet] The Prophet Muhammad's (PBUH) Last Sermon
To: "Feisal Amour" <famour@hotmail.com>, zanzinet@zanzinet.org
Assalamun alaikum ndugu Faisal
Naona ndugu umeleta hadith ingine kwa madhumuni ya kuipinga hii hadith ya Kitabu na Itrati Ahlel Bait. Hukuonesha dalili yeyote wala uzito wake yakuifanya hiyo hadith ya Kitabu na Sunnah iweze ikubalike. Kinyume chake hadith ya Kitabu na Itrati inayo Uzito na yenye kukubalika zaidi na sababu yenye kama ifuatayo:-
1) Siyo hadith zote zilizoletwa na Masahaba ni ya kweli. Walikuwa baadhi yao wakimsingiziya mtume (s.a.w) uwongo katika uhai wake, na kuna hadith zingine zina maana zaidi ya moja, zipo hadith zingine zimekuwa batil lakini masahaba wengine walikuwa hawana habari, zipo hadith zingine kwa wakati wake maalum na kazalika. Khalifa wa mwanzo na wapili wakipinga kwa kukusanywa hadith na ngapi wameziunguza. Tuchukuwe mfano wa sala, baada ya mtume (s.a.w) masahaba wenyewe kwa wenyewe wakiikhtilifiana namna ya kusali ambae walikuwa wakisalai pamoja na mtume (s.a.w) kiasi ya miaka 23 na bado wakiikhitilifiana. Sasa ikiwa mambo kama hayo vipi tena mtume (s.a.w) awaambiye yakuwa mkiufuata Quran na Sunnah kabisa hawatapoteya? Hiyo Sunnah gani mtume (s.a.w) akizungumzia, ikiwa sala wakiikhitifiana, wengine wakimsingiziya uwongo, hadith zingine zenye maana ngapi na kazalik?
2) Ingekuwa hiyo hadith ya Kitabu na Sunnah kweli inayo uzito na yenye kukubalika, basi leo tusingeona hayo madhehebu katika Uislamu, kwasababu hayo yote tafauti yetu inatokana na kutofahamu vizuri Kitabu cha Allah na Sunnah ya Mtume (s.a.w), vipi tena itatuongoza?
Tukitizama Quran, kila moja anayo tafsir yake na anafuata anavyo amini yeye ndiyo sawa. Tukija kwenye Sunnah hiyo vishindo zaidi, kwa sababu siyo tunahitajiya dalil ya hiyo hadith hata Asnad waislamu wanatafautiyana. Sasa ikiwa hiyo tafauti ya Waislamu ipo kuifahamu hiyo Quran na Sunnah vipi tena tutaikubali hiyo hadith?
3) Tukiitizama hii hadith ya Kitabu ya Allah na Sunnah haina uzito hata iwe ndiyo yenye kuaminika. Hii hadith hutoweza kuipata kwenye vitabu vya SAHIH isipokuwa kwenye Muwatta ya Malik. Na katika Muwata haina Asnad kuelezea hiyo hadith nani ameileta, isipokuwa Imam Malik mwenye ameitamka ambae yeye mwenyewe amekuja baada ya zaidi miaka miya ya mtume (s.a.w). Hadith kama hizi zinajulika kuwa ni DHAIFU.
4) Hadith ya Kitabu na Itrati imeelezwa na masahaba zaidi ya 25 kwa njia tafauti, na inajulikana yakuwa hadith yenye kuletwa na sahaba watano huwa hadith hii ni MUTAWATIR. Basi hadith hii imepindukiya masahaba 25, hadith ya Mutawatir ni yenye Uzito wa juu kama aya ya Quran!
5) Quran ni kama Bustani au mji iliyopambwa yenye kila aina ya njiya. Ukitaka kwenda kuchuma aina yeyote ya tunda kwenye bustan lazima utakuwa unahitajika na Muongozi mwenye kukuongoza na kukuonesha tunda gani ipo wapi. Au ukifika kwenye mji lazima upate Muongozi ya kukuonesha njiya gani kutumiya kutaka kufika mahali fulani. Basi Quran bila ya Muongozi ndiyo tutapata shida ya kuifahamu kama hali ya sese hivi, kila moja huamini tafsir yake ndiyo sawa.
6) Na Sunnah ya Mtume (s.a.w) inahitajiwa kuhifadhiwa na Kiongozi ambae atayetupa hadith ya ukamilifu ya Mtume (s.a.w) kama alivyosemana mwenyewe bila ya kupunguwa au kuzidi. Siyo kama hadith tuliyokuwa nazo
ambazo zinakhatalifiana na asnad zingine zisizokubalika.
Basi hao VIONGOZI ni hao Itrati Ahlel Bayt ambaye kazi yao ni kutufundisha mafunzo ya sawa ya Quran na ya Sunnah ya Mtume (s.a.w). Basi hadith ya Quran na Itrati Ahlel Bait ni yenye Mantaqi na yenye kukubalika siyo Quran na Sunnah!
Wassalam
Mohammed Yusuf
05/12/2001
--- Feisal Amour <famour@hotmail.com> wrote: