Date: Sun, 03 Oct 99 13:33PM MDT
From: "Mohammed Y.Jaffer" <abulqassim@usa.net>
To: zanzinet <zanzinet@zanzinet.org>
Cc: abulqassim@usa.net
Subject: [zanzinet] Re: [Re: Utukufu Wa Mtume Muhammad (s.a.w)]
HADITH ZA UPUZI
Maneno ya Mohammed Faraj
"Ama kuhusu uwezo wa Mitume (AS) kuwaingilia wanawake zaidi ya 30, sijui
maneno hayo yametokea wapi, lakini mimi sikuyasema maneno hayo. Lakini
ukitaka nizungumzie juu ya uwezo wa Mitume (AS) kufanya hayo basi nitanukuu
kutoka katika vitabu vyenu vitukufu vya Kishia vilivyoandikwa na Maulamaa
wenu;
Katika kitabu kiitwcho AL Burhan 4/49 na kitabu cha Furu-u l Kafi 5/567
imeandikwa hivi;
"Kutoka kwa Hasan bin Jaham anasema; ' Abil Hasan alinambia;
"Suleiman bin Daud alikuwa na wake elfu moja ndani ya kasri yake ......
(mpaka mwisho wa hadithi akasema) "ALikuwa akiwaingilia kila usiku"
Na imenukuliwa kutoka kwa Neemat AL Jazairi(naye pia ni Mshia) kutoka
katika
kitabu cha "QIsasul Anbiyaa" ukurasa wa 407, na hiki ni kitabu cha Mashia .
Imenukuliwa kuwa;"
Maneno yangu
Mimi sikusema yakuwa hayo maneno amesema yeye, nimeleta kwa kutaka kuongeza nguvu hoja yangu.
Hizo vitabu alizozitaja sisi hatuzitambu kuwa ni VITABU SAHIH, SASA MIMI NIMESHAYAKATAA
HIZO HADITH YAKUWA DHAIFU, BASI MWACHE NA YEYE AFANYE KAMA NINAVOFANYA
MIMI. Haina haja ya kwenda juu chini kutaka KUITETEA HADITH ZA UPUZI NA ZA UWONGO KUHUSU
MTUME WETU (S.A.W) AU MITUME WENGINE. BADILI YA KUMTETEA MTUME WETU (S.A.W)
NAONA NDUGU AMECHAGUWA KUTETEA HIZO HADITH, MAMBO YA KUSTAAJABISHA!
SIFA ZA ALI (A.S)
Maneno ya Mohammed Faraj
Sifa za ALi bin Abi Talib(RA) Kuhusu sifa zenu mnazompa Sayiduna Ali Bin Abi Talib(RA) zisizoweza kukubalika
na yeyote mwenye akili timamu , hilo ni shauri lenu. Na haya hamjaanza nyinyi, maana kabla yenu alikuwepo
Myahudi mmoja aitwae Abdillahi bin Saba-a aliyeingia katika dini hii kwa nia ya kutaka kuifisidi. Huyu ni katika
Mashia wa mwanzo wa ALi(RA), na mtu huyu alipindukia mpaka katika kumsifia ALi(RA) hata akafikia
kumwambia ALi kuwa yeye ni Allah, na Ali(RA)akamhukumu kuuyliwa kwa kumchoma moto kwa ajili ya kufru
yake hiyo. Soma kitabu cha AL Hilmy ukurasa wa 164 juzu ya 2 (hiki pia ni kitabu cha Kishia).
Maneno yangu
Hapa ndugu ameleta mada mbili pamoja, ya mwanzo kuhusu hadith zinazomhusu Imam
Ali (a.s) na yapili kuhusu Abdullah ibn Saba.
HADITHI KUMHUSU IMAM ALI (A.S)
Bado ndugu anaendelea kunistaajabisha. Ikiwa ninapoletea hadith kuhusu Imam
Ali (a.s) zaidi ninatowa kwenye vitabu vyenu ambae hadith ngapi zingine ni
Mutawwatir na kukubaliwa na Maulama wa Kisunni.
ABDULLAH BIN SABA
Mwenye kuleta hadith kuhusu Abdullah bin Saba ni Sayf Ibn Umar al-Dhabbi
al-Usayyidi al-Tamimi, ambae amefariki katika 170 AH, katika wakati wa Haroon
al-Rashid. Sayf ameandika vitabu viwili ambae ilikuwa inapatikana wakati wa
hukum ya Bani Ummaya. Vitabu vyenyewe ni "al-Fotooh wa al-Riddah" inaelezea
tarikh kutoka kabla kufariki Mtume (s.a.w) mpaka wakati wa Khalifa wa tatu. Na
kitabu cha pili ni "al-Jamal wa Maseeri Aisha wa Ali" inaelezea tarikh kutoka
uwaji wa Uthman mpaka vita ya Jamal.
Huyu jamaa Sayf anajulikana kuwa ni MUONGO NA MWENYE KUTUNGA HADITH ZA UWONGO,
KAMA HADITH ZA ELFU LAILA WA LAILA. Maualam maaruf wa Kisunni wamethibitisha yakuwa
huyu Sayf ibn Umar alikuwa Maarufu mwenye kujulikana kwa Kusema UWONGO, kama al-Hakim,
al-Nisa'I, Yahya Ibn Mueen, Abu Hatam, Ibn Abi Hatam, Abu Dawud, Ibn Habban, Ibn Abd al-Barr,
al-Darqutini, Firoozabad, Ibn al-Sakan, Safi al-Din, Ibn Udei, al-Suyuti and Ibn Hajar al-Asqalani.
Hata hiyo kitabu ya Kishia iliyoandika kuhusu huyu Abdullah bin Saba haipo katika vitabu nne maaruf.
Kitabu al-Kushshi ameleta hadith nyingi dhaifu na isiyokubalika. Tuseme yakuwa kweli huyu mtu
alikuwepo na ameunguzwa na Imam Ali (a.s), sasa itakuwa ndio nini? Maulama wa Kishia wanamehaesabu
huyu Abdullah ibn Saba ni Munafiq. Ikiwa mtu Munafqi ametokeza kuwa rafiki wa Ali
(a.s) atakuwa anayo kitu gani yakumfanya yeye awe Shia? Ikiwa Mwizi amepanda
kwenye Mimbar na ameleta athari mbaya na kuharibu jina la Islam, je na sisi
tuwachukiye hao Maulama na tuwaite ni Wezi?
Ukisoma hiyo hadith ya Elfu laila wa laila ya huyu Sayf utaona hata Masahaba
wakubwa ambae walikuwa wakijulikana kuwa Shiatu Ali kama Abu Dhar na Ammar
Yasir walikuwa wanafunzi wa huyu Abdullah ibn Saba. Jee inaingia akilini watu
hao wamuache Ali (a.s) na kuenda kumfuata huyu Myahudi, na hali wao ndio wenye
kusikia hadith za Mtume (s.a.w) kuhusu Ali (a.s)?
Naona ndugu yetu atatafuta kila chochote mbaya apate kuwapachika hao Mashiya hata ikiwa ya Uwongo
na kuwacha ya Ukweli. Nitapenda ndugu yetu awache kuleta hizo hadith za UWONGO NA KULETA HADITH
ZA UKWELI, KWA MFANO YA KAAB AL-AHBAR. Nitapenda atueleze huyu RABBI YAKIYAHUDI
ALIYEKUWA KARIBU NA KHALIFA WA PILI NA WATATU, NA VIPI WAO WAKICHUKUWA
SHAURI YAKE. SIO KUTULETEA HADITH ZA ELFU LAILA WA LAILA YA SAYF AL-KAZAB!!!!!
Wassalam
Mohammed Yusuf
Date: Tue, 05 Oct 99 05:31AM MDT
From: "Muhammad Aly" <muhammadaly@hotmail.com>
To: abulqassim@usa.net
Cc: zanzinet@zanzinet.org
Subject: Re: Utukufu Wa Mtume Muhammad (s.a.w)(nyongeza)
Bismillah
Assalam Alaykum
Wananeti wote, ………………
Huko kutaja kwako kwa Abdullah Bin Sabaa kunastaajabisha, wewe ni mtu wa Elimu, mambo mengine hayafai
kuambiwa, habari za Abdullah Bin Sabaa Sheikh Mohammed Faraj zimepitiwa na wakati na umeshaelezwa humu
lakini kwa kukuongezea tu, mtu huyu hakupata kuishi Duniani, na habari zake zote ni uzushi wa huyo
Saif Bin Omar At-Tamimi, ukitaka kujuwa zaidi ya ukweli wa maneno haya, Maulamaa wa Kiislamu wengi
waliotabahari kwenye Ellimu za Tariikh wanaona kuwa mtu huyu hakluwepo bali hiyo ilikuwa ni silaha moja wapo
ya kutaka ama kunusuru heshima ya masahaba ama silaha dhidi ya nguvu ya Ushia uliowapa tabu kisiasa na
kijamii watawala wa kibanu Umayyah na wengineo...Hivyo kwa ajili hii Maulamaa wa Kisunni na wa Kishia wamekataa
kuwepo kwa mtu huyu kwa hoja madhubuti zilizochukuliwa kwenye Vitabu vyote unavyovijuwa na usivyovijuwa
vya Tariikh ya Kiislamu...Tazama ushahidi wa haya kwenye:
(i) Kitabu "Abdullah Bin Sabaa, cha Allamah Seyyid Mortadha Al-Askari. na kwa wanavyuoni wa Kisunni soma
(ii)Kitabu "Adullah Ibn Sabaa: A Study Of the Historical Resources Concerning His Role in Al-Fitnah" cha
Sheikh Abdul-Aziiz S. Al-Helaabi, Dean wa Kitivo cha Tariikh kwenye King saud University- Saud Arabia..
(iii)Kitabu " Adh'waa ala Sunnati Muhammadiyyah" cha Sheikh wa Azhar miaka ya 1950s Mahmoud Abu-Rayyah
na kadhalika..
Tanbihi: Dalili zilizomo kwenye Vitabu hivi zitakutosha na huhitaji hoja nyengine zo zote na baada ya kusoma
Vitabu hivi nakuomba utuletee maoni yako juu ya habari za huyu Abdullah Bin Sabaa mnayedai kwa kutegemea
Hadithi za waongo akina (Saif Bin Omar tamimi) ambaye mimi namwita "Bunuwasi" wa hadithi kama Wanavyuoni
wote wa Kishia na Kisunni wanavyomwita, umeona listi ya wanavyuoni wa Kisunni walivyomkataa
Seif Bin Omar tamimi kwenye makala ya bwana Mohammed Yussuf Jaffer, tunaomba wananeti watafakari kwenye
mambo ya hakika na wayatupilie mbali mambo yaliyopitiwa na wakati...
Ahsanteni,
Samahani kama nimetumia lugha mbaya, naomba samahani kwa wananeti wote....Ndugu yenu, Muhammad Aly.