Hii ifutayo ni mfano ya hiyo matunda ya ile mbegu iliyopandwa na site ya mawaidha :

 

Muhammad Faraj    Thu 12/04/01 19:45            [zanzinet] Re: Ukumbi mpya!/Darsa za Sh. Muhammed Faraj   

 

 

Ndugu zangu Waislam

Assalaam alaykum wa Rahmatullahi wa Barakatuh

Namshukuru Ustadh Peku namshukuru Ndugu Muhammad Al Suqry nawashukuru pia wote wale wanaoniandikia binafsi mara kwa mara kwa kunipa moyo wa kuendeleza darsi humu wavuni na namshukuru pia Sheikh Farouk Abdullah Amour kwa nasaha zake na dua zake za mara kwa mara, nakuhakikishieni nyote pamoja na ndugu wengine kuwa daima nitajaribu kuleta yale yenye manufaa kwa Waislam wote, yale yenye kutuelimisha na kutuunganisha na kutufurahisha na si yale yenye kutupotosha na kututenganisha na kutughadhibisha. Hata hivyo mimi ni binadamu na wakati mwingine huchukuliwa na hamasa kutokana na baadhi ya mijadala  inavyoendeshwa humu na huenda likanitoka neno hapa au pale.

Nakaribisha masahihisho ya kujenga wakati wowote ule.

Haadha wallahu waliyyu ttawfiyq

Wa ssalaam alaykum wa Rahmatullahi wa Barakatuh

Ndugu yenu

Muhammad Faraj Salem

 

Sasa wache tutizame ile site yake yenye kuja upotofi, uwongo, uadi na ukhasama nini imeleta NATIJA YAKE katika ukumbi wa Zanzinet. Eti kweli ndugu yetu anataka “daima nitajaribu kuleta yale yenye manufaa kwa Waislam wote, yale yenye kutuelimisha na kutuunganisha na kutufurahisha na si yale yenye kutupotosha na kututenganisha na kutughadhibisha”

 

 

Amour Nasser            Sun 10/03/02 09:55            [Zanzinet] Ni kweli Shiaa wanaamini hivi?

 

Assalamu Alaykum,

 

Maandishi haya yanapatikana toka:

 

http://www27.brinkster.com/mawaidha1/fatwa.htm

 

++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

 

1.  AHLIL BAYTI HAWAIHITAJII QURANI KWA SABABU WANA

VITABU VYA MWENYEZI MUNGU VILIVYOTANGULIA KUTEREMSHWA

NAVYO NI TAURATI NA INJILI

 

Ukweli huu unathibitishwa na yale yaliyoandikwa katika

kitabu cha Al Kaafi Juzuu ya kwanza Kitabul Hojjah

ukurasa wa 207.

 

2.  KUITAKIDI KUWA HAPANA SAHABA YEYOTE ALIYEWAHI

KUIKUSANYA AU KUIHIFADHI QURANI TUKUFU ISIPOKUWA ALI

NA MAIMAM WA AHLI L BAYT (RA) PEKE YAO.

 

Itikadi hii imethibitishwa katika kitabu cha Al Kaafi

Juzuu ya kwanza kitabu cha Al Hojjah ukurasa wa 26.

 

3.  ITIKADI KUWA AHLI LBAYT NA WAFUASI WAO WANA ELIMU

YA MITUME NA YA MWENYEZI MUNGU WASIOKUWA NAYO WAISLAM

WENGINE

 

Uhakika huu umeelezwa katika kitabu cha Al Kaafi Juzuu

ya kwanza kitabu cha Al Hojjah Ukurasa wa 138.

 

4.  KUITAKIDI KUWA MASAHABA WA MTUME (SAW) WOTE (RA)

WAMERTADDI NA KUKUFURU BAADA YA KUFA KWAKE ISIPOKUWA

AHLI L BAYTI NA WENGINE WACHACHE KAMA VILE SALMAN NA

AMMAR NA BILAL (RA.

 

Ama ushahidi wa ukweli huu na ili kuupata uhakika

wake, tunakuleteeni dalili zifuatazo;

 

1- Katika kitabu cha Roudhatul Kaafi cha Al Kilaniy

mwenye kitabu hiki cha Al Kaafi, ukurasa wa 202.

 

5.  ITIKADI KUITAKIDI KUWA MAIMAM WA MASHIA, DARAJA

LAO NI SAWA NA DARAJA LA MTUME (SAW) KATIKA KUKINGWA

ILI WASIFANYE MADHAMBI WALA MAKOSA NA PIA KATIKA

KUFUNULIWA WAHYI NA KATIKA KUTIIWA (TA-A) NA MENGINE .

ISIPOKUWA KATIKA KUOWA, WAO HAWARUHUSIWI KUOWA KAMA

ALIVYORUHUSIWA MTUME(SAW).

 

Itikadi hii inayowapandisha Maima wa Kishia kuifikia

daraja ya Mtume(SAW), imeandikwa na kuthibitishwa na

mwandishi wa kitabu cha Al Kafi kwa kuegemea ushahidi

wake kutoka katika riwaya mbili.

 

YA KWANZA; Hadithi iliyosimuliwa katika ((kitabu cha

Al Hojjah - ukurasa wa 229;pale aliposema;

 

"Al Mufadhal alikuwa kwa Abu Abdullah akamuuliza;

 

"Nimejitolea mhanga kwa ajili yako, ni kweli kuwa

Mwenyezi Mungu anaweza kuwafaridhishia watu kumtii mtu

kisha akamzuilia mtu huyo kheri itokayo mbinguni?

 

Abu Abdillahi (katika maimam wa Mashia) akamjibu;

 

"La- Mwenyezi Mungu ni Mkarimu na Mwenye Huruma na

Mpole zaidi kwa waja Wake, hawezi kuwafaridhishia waja

wake kumtii mtu, kisha amzuwilie mtu huyo kheri

itokayo mbinguni asubuhi na jioni".

 

YA PILI; Hadithi iliyosimuliwa katika ((Juzuu ya

kwanza ya kitabu cha Al Hojjah - ukurasa wa 229)).

 

Amesema;

 

'Kutoka kwa Muhammad bin Salem, amesema; "Nimemsikia

Aba Abdullah alayhi Ssalaam akisema;

 

"Maimamu daraja lao ni sawa na daraja la Mtume(SAW),

isipokuwa wao si Mitume na hawaruhusiwi kuowa kama

alivyoruhusiwa Mtume(SAW). Ama kwa mengine yasiyokuwa

hayo, daraja lao ni sawa na la Mtume(SAW)".

 

 

 

__________________________________________________

Do You Yahoo!?

Try FREE Yahoo! Mail - the world's greatest free email!

http://mail.yahoo.com/

 

_______________________________________________

Zanzinet mailing list

Zanzinet@zanzinet.org

http://www.zanzinet.org/mailman/listinfo.cgi/zanzinet

 

 

Hashim Sun 10/03/02 15:56            Re: [zanzinet] Ni kweli Shia wanaamini hivi?

 

Assalaam Aleykum

Wananeti

Haya mambo uloyaleta Sheikh Nasser Amour kutoka katika hiyo site ya Mawaidha, mimi binafsi nimeshaitembelea na nikaona vituko kama hivi, na nikaiuliza nafsi yangu “huyu aloandika haya ameyapima na kuzingatia aliyoandika au kuipa jina la hiyo site Mawaidha ni kweli site hii ina mawaidha na kufundisha watu mambo muhimu katika Uisilamu?” Ukweli wa mambo mimi sikuona ila kitu kimoja tu nacho ni kuupaka mavi Ushia kwa kadri alivyotaka yeye Sheikh M. Faraj. Ni vizuri kuzungumza akida za mwenzako lakini iwe kwa njiya ya hekma bila ya kusababisha vurumai kwa wale wanao amini akida hiyo.

Mawahabbi wamejitihad kwa kiasi chao kuuponda ushia lakini hawakuweza kufaulu na hili linajulikana wazi kwa waisilamu. Walofaulu khasa ni hawa wanaopondwa na kupewa kila majina wasostahiki kupewa, Shia Ja’afari. Tuhma zao wanazowatuhumu huwa zinawapa nguvu sana Mashia, kwasababu mtu anapoyasikia haya huwa anataka kwenda chini zaidi ili aujue huu Ushia. Ikifikia hadi hii, mtu huyo hubadilika zile fikra zake na kuona yale alokuwa akiyasikia hayako kwa Mashia, hapo tena mwenye kubadili Madhehebu atabadili na mwenye kuachia kama yalivyo ataachia lakini siku zote ukweli haupingiki utabaki pale pale.

Ndugu Nasser Amour, mimi najaribu kuyajibu haya mambo uloyaleta, na Inshaallah yataweza kukusaidia na kukupa mwanga.

 

Kutoka Site ya Mawaidha

  1. AHLIL BAYTI HAWAIHITAJII QURANI KWA SABABU WANA
    VITABU VYA MWENYEZI MUNGU VILIVYOTANGULIA KUTEREMSHWA
    NAVYO NI TAURATI NA INJILI.

    Ukweli huu unathibitishwa na yale yaliyoandikwa katika
    kitabu cha Al Kaafi Juzuu ya kwanza Kitabul Hojjah
    ukurasa wa 207.

Majibu Yetu

Hii, ni moja katika tuhma alokuja nazo ndugu M.Faraj. Maneno haya hayana msingi hata kidogo na hata ukamuambia mtoto wa miaka 6 atakucheka. Sikuweza kuamaini kweli maneno haya ataweza kuyaweka kwenye site yake, nilivofahamu mimi si kitu chengine ila kutaka kuupaka mavi Ushia, kwa hili nasema halini athari yoyote kwa Shia.

Ndugu Nasser Amour, kwanza napenda ufahamu jambo moja na tena muhimu sana kulielewa kwasababu kama utasoma maneno kama haya ya ki upuuzi basi unaweza kutekwa ikiwa hutotumia uangalifu. Hayo yaloandikwa na ya katolewa kwenye kitabu cha Kishia ambacho kitabu hichi hujulikana kwa Mashia kitabu kikubwa baada ya Qur’an. Hata hivyo juu ya ukubwa wake, hakuna Shia yoyote yule ambae anaweza kuthibitisha au kuthubutu kusema kama kitabu na hadithi zilizomo ndani yake ni Sahih. Hadithi zilizopokelewa kwenye kitabu hichi natumai s chini ya 17.000, lakini zaidi ya asilimia 50 (50%) ni dhaifu, yaani kama hadithi 5000 na kidogo hivi zinakubaliwa kuwa ni sahih. Vile vile, huyu bwana alozipokeya hizi hadithi amesema katika Muqadima wa kitabu chake cha al-Kafi kuwa ichukuwe hadithi na uipime kwenye mizani ya Qur’an na utakapoona kuwa haikubaliani na Qur’an, basi itupilie mbali. Sasa ndugu Nasser Amour, kweli hadithi kama hii itaweza kukubaliana na Qur’an? Jibu, haikubaliani na Qur’an, na kama ni hivi, ilikuwaje ikanukuliwa na kusomeshwa watu? Hivyo ndugu Nasser, Imani hii haipo kabisa kwa Mashia

Kutoka Site ya Mawaidha


2. KUITAKIDI KUWA HAPANA SAHABA YEYOTE ALIYEWAHI
KUIKUSANYA AU KUIHIFADHI QURANI TUKUFU ISIPOKUWA ALI
NA MAIMAM WA AHLI L BAYT (RA) PEKE YAO.

Itikadi hii imethibitishwa katika kitabu cha Al Kaafi
Juzuu ya kwanza kitabu cha Al Hojjah ukurasa wa 26.

Majibu yetu

Hili pia sio kweli, ila tu Mashia wanasema kuwa Imam Ali (a.s.) alikusanya na kuhifadhi Qur’an kwa mpangilio wa aya au sura zilivyoteremka. Shia pia wanaamini kuwa, wapo Masahaba walokusanya na walohifadhi Qur’an. Haya yamethibitishwa kutoka kwenye vitabu vya kisunni kuwa wapo baaaadhi ya Mashaba walikuwa wamekusanya Qur’an kwa njiya tafauti, sina haja ya kusema yapo wapi kwani yajulikana vizzuri sana.

Kutoka Site ya Mawaidha

3. ITIKADI KUWA AHLI LBAYT NA WAFUASI WAO WANA ELIMU
YA MITUME NA YA MWENYEZI MUNGU WASIOKUWA NAYO WAISLAM
WENGINE

Uhakika huu umeelezwa katika kitabu cha Al Kaafi Juzuu
ya kwanza kitabu cha Al Hojjah Ukurasa wa 138.

Majibu Yetu

Tuhma hii haikubaliki asilan ni uzushi wa kiWahabbi kutaka kuwapaka mavi Mashia. Imani ya Ki-Shia juu ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake iko wazi kabisa isipokuwa kuna khitilafu wanavoamini masunni na tena sio wote kuwa Siku ya hesabu Mungu ataonekana lakini Mashia wanasema kuwa Mungu haonekani hapa duniani wala Akhera abadaan, wana sababu zao hata wakasema hivi.

Allah ni Mwalimu wa Mtume (s.a.w.), Ahli Bayt ni wanafunzi wa Mtume, sasa vipi Mungu na Mtume watakuwa sawa kwa elimu zao na hawa Ahli Bayt? Mambo gani haya ndugu zangu? Mtu wa kuaminika unaweka mambo ya kiupuzi kwenye site yako na hapo hapo umeipa jina la site hiyo inayojulikana kwa jina la Mawaidha? Haifai kuweka mambo yasokuwa na maana kama haya ambayo siku zote yanaleta su’u tafaham kwa jamia ya Waisilamu

Kutoka site ya Mawaidha

4. KUITAKIDI KUWA MASAHABA WA MTUME (SAW) WOTE (RA)
WAMERTADDI NA KUKUFURU BAADA YA KUFA KWAKE ISIPOKUWA
AHLI L BAYTI NA WENGINE WACHACHE KAMA VILE SALMAN NA
AMMAR NA BILAL (RA.

Ama ushahidi wa ukweli huu na ili kuupata uhakika
wake, tunakuleteeni dalili zifuatazo;

1- Katika kitabu cha Roudhatul Kaafi cha Al Kilaniy
mwenye kitabu hiki cha Al Kaafi, ukurasa wa 202.

Majibu yetu

Shia wana amini kuwa sio Masahaba wote waadilifu, kuna wenye walotenda Mema na kuna walotenda maovu. Hivyo kila Sahaba atahukumiwa kwa Matendo yake kama ni maovu au mazuri.

Kuhusu kuratadi kwa Sahaba, kwanza, inatupasaa tujuwe definition ya Sahaba. Nani Sahaba? Sahaba ni yule alomuona Bwana Mtume Muhammad (s.a.w.) na akasilimu na kufa yuhali yumo kwenye uisilamu, hichi ni kielezo sahihi cha Sahaba. Kuna Masahaba ambao wameritadi wakti Bwana Mtume yuhai, kuna Masahaba wamertadi baada kufa Bwana Mtume (s.a.w.). Sasa kwanini tunashangaa ikiwa tunayapata haya katika vitabu vya kisunni ambavyo vya kuaminika?

Lakini si kweli kama alivyotuambia ndugu M.Faraj kuwa Masahaba wote wamertadi japo kuwa amenukuu kutoka katika kitabu hicho alichokishikilia cha al-Kafi, kwasababu si kila kitu kilichomo ndani ya kitabu hiki ni sahih. Hivyo ndugu Nasser, mambo mengine yanataka kweli kuzangatia kwasababu baadhi ya Mashekhe wengine wanapenda sana kutuchezea shere, tuwe careful katika kuya judge mambo kama haya

Kutoka Site ya Mawaidha

5. ITIKADI KUITAKIDI KUWA MAIMAM WA MASHIA, DARAJA
LAO NI SAWA NA DARAJA LA MTUME (SAW) KATIKA KUKINGWA
ILI WASIFANYE MADHAMBI WALA MAKOSA NA PIA KATIKA
KUFUNULIWA WAHYI NA KATIKA KUTIIWA (TA-A) NA MENGINE .
ISIPOKUWA KATIKA KUOWA, WAO HAWARUHUSIWI KUOWA KAMA
ALIVYORUHUSIWA MTUME(SAW).

Itikadi hii inayowapandisha Maima wa Kishia kuifikia
daraja ya Mtume(SAW), imeandikwa na kuthibitishwa na
mwandishi wa kitabu cha Al Kafi kwa kuegemea ushahidi
wake kutoka katika riwaya mbili.

Nimeshaelezea hapo mwanzo kuwa daraja ya Mtume (s.a.w.) na Ahli Bayt haiwezi kuwa ni daraja zao kuwa ni sawa, hata hivyo kuna nyongeza kuhusu utukufu wa Ahli Bayt.

Shia wana amini kuwa Mwenyezi Mungu amewahifadhi Ahli Bayt na kila aina ya maovu. Ushahidi wanao utegemea ni kutoka kwenye Qur’an Sura ya 33 Ahzab aya ya 33, hapo utaona haya nilosema ya kuhifadhiwa kwa Ahli Bayt.

Ama Ahli Bayt kuteremshiwa wahyi, sijapata kusikia na ndio kwanza nasikia hii leo, hata hivyo hakuna la ajabu kwani ukiangalia Qur’an utaona pia Nyuki ameteremshiwa wahyi, Bibi Maryam, mama wa Nabi Issa ameteremshiwa Wahyi na yeye alikuwa si Mtume, au kuna Wahyi mwengine ambao hatufahamu sisi?

 

 

 

Jaffer, Mohammed TCI63  Sun 10/03/02 16:01            RE: [Zanzinet] Ni kweli Shiaa wanaamini hivi?

Amour

 

Baada ya kupitiya hii site ya Wahabi ambaye mengi ndani yake tuliwahi kujadili hapa ukumbini basi nae tembeleya site hii :

 

http://www.answering-ansar.org/

 

 

Usisahao tumeshasema mara nyingi yakuwa siyo kila iliyomo kwenye vitabu vyetu ndiyo imani yetu. Kitabu yenye kukuablika bila makosa na yenye kufuata bila kuulizwa ni Quran tu!

 

Ikiwa kila hadith iliyomo kwenye vitabu vya hadith in Iman, basi kuna mengi yakusema kwenye vitabu vyenu. Na sisi tunaweza kuleta hapa ukumbini!

 

Wassalam

 

Mohammed Yusuf

 

 

 

Mohamed Faraj    Sun 10/03/02 23:14            Re: [zanzinet] Ni kweli Shia wanaamini hivi?

Assalaam alaykum wa Rahmatullahi wa Barakatuh

Kwanza kabisa siye mimi niliyeyaingiza maudhui haya ukumbini humu.

Pili sitopenda kuendelea kujadiliana ndani ya ukumbi huu kwani uwanja mwingine ulikwisha tengwa tokea zamani kwa jili ya majadiliano yanayohusu madhehebu.

Tatu kuhusu kukanusha kwako na kuzidhoofisha hadithi za Al Kafi kilichoandikwa na aalim mkubwa wa Kishia kama Al Kulliniy na kunambia kuwa mimi naupaka mavi Ushia, naona kauli yako hiyo si ya haki kwani mimi hadithi hizo zikuzitoa akilini mwangu bali nimezitoa ndani ya vitabu vyenu ambavyo ndani yake haikuelezwa juu ya usahihi au udhaifu wake - Bila shaka umetumia elimu fulani hata ukaweza kupata natija ya kuwa asilima 50 ya hadithi zilizomo ndani ya Al Kafi ni za uongo, na kwa ajili hiyo ningependa unijulishe ni njia gani ya kielimu ninayoweza na mimi kuitumia ili niweze kuzijuwa hizo hadithi za uongo zilizomo ndani ya vitabu hivyo ili niweze kuepukana nazo.

 

Ndugu Hashim mimi nimesoma comments nyingi za maulamaa wenu juu ya kitabu hiki cha Al Kafi na wamekisifia sana kupita kiasi na chini hapa nakutilia baadhi tu ya kauli hizo mojawapo ikiwa ni ya Al Kulliny mwenyewe katika muqaddimah ya kitabu chake hicho.

 

Kama huna kitabu hicho basi unaweza kuzipata comments hizo kwa urahisi katika site yenu na anuani yake ni;

Al-shia.com.- upande wa kiarabu ukurasa wa ‘kutub’.

Nne, kama hadithi hizo ni za uongo kama unavyosema, basi mbona wanaendela kupiga chapa tu vitabu hivyo kila siku tena bila kuwajulisha watu juu ya uongo uliomo ndani yake. Maana unapofungua kitabu na kusoma hadithi hizo huoni mahali popote panapoandikwa kuwa hadithi hizo ni dhaifu, basi sijuwi wewe mwenzangu umefanya wapi tahakiki hiyo?


Ndugu Hashim kumbuka kuwa mlileta hadithi ya Nabii Musa (AS) na namna Mwenyezi Mungu alivyojaalia jiwe liondoke baada ya kuweka nguo zake juu yake mkatuambia kuwa sisi tunafuata hadithi za uongo – lakini tulipojaaliwa kupiga mbizi ndani ya vitabu vyenu na kuona kuwa na humo pia hatdithi hiyo imeandikwa mkasema maneno haya haya kuwa vitabu vyetu ni vya uongo.

 

Maudhui ya funga ya Ashura mlituambia kuwa tusifunge na kwamba ni haramu na kwamba si katika sunnah ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW), nakwamba eti Yazid ndiye aliyeitunga saumu hiyo, na baada ya kufunguwa vitabu vyenu na kuona kuwa na humo pia imeandikwa juu ya saumu hiyo na kwamba Imam Ali (RA) alikuwa akihimiza watu kufunga saumu hiyo mlinyamaza na wengine wakasema maneno hayo hayo kuwa hadithi zetu ni dhaifu.

 

Sasa ikiwa hadithi zenu zote ni dhaifu si bora mnyamaze na muache kushambulia madhehebu ya watu?

 

Leo mnatuambia sisi pagans tunaamini kuwa Nabii Issa alipaishwa mbinguni, kesho mnatuambia kuwa sisi ni wapotofu tunawafuata Abubakar na Omar mara mnatuambia kuwa Imam Bukhari na Muslim ni waongo.

Kwa nini basi hamufungi mijadala huu tukakaa raha mustareh kila mtu na madhehebu yake ?

Al Kullini katika Muqaddimah aliandika ifuatavyo;

“Nimeandika kitabu hiki ili kama mtu atapenda awe na kitabu kilichojumuisha fani zote za elimu ya dini kitakachomtosheleza mwanafunzi na kiwe marejeo kwa mwenye kutaka uongofu ili achukuwe ndani yake anachotaka katika elimu ya dini na kuifanyia kazi na kitabu hicho kiwe ni dalili zilizo wazi kutoka kwa wasemakweli.

Ama Attubrusiy yeye anasema ifuatavyo;

“Al Kafi baina ya vitabu vinne ni mfano wa juwa baina ya nyota"

Al Kashani na wengi miongoni mwa maulamaa wengu wamekisifia sana pia kitabu hicho lakini sitaki kuwachosha wasomaji.

Wallahu taala aalam

Wassalaam alaykum wa rahmatullahi wa Barakatuh

Muhammad Faraj Salem

 

Ndugu Nasser Amour, kwanza napenda ufahamu jambo moja na tena muhimu sana kulielewa kwasababu kama utasoma maneno kama haya ya ki upuuzi basi unaweza kutekwa ikiwa hutotumia uangalifu. Hayo yaloandikwa na ya katolewa kwenye kitabu cha Kishia ambacho kitabu hichi hujulikana kwa Mashia kitabu kikubwa baada ya Qur’an. Hata hivyo juu ya ukubwa wake, hakuna Shia yoyote yule ambae anaweza kuthibitisha au kuthubutu kusema kama kitabu na hadithi zilizomo ndani yake ni Sahih. Hadithi zilizopokelewa kwenye kitabu hichi natumai s chini ya 17.000, lakini zaidi ya asilimia 50 (50%) ni dhaifu, yaani kama hadithi 5000 na kidogo hivi zinakubaliwa kuwa ni sahih. Vile vile, huyu bwana alozipokeya hizi hadithi amesema katika Muqadima wa kitabu chake cha al-Kafi kuwa ichukuwe hadithi na uipime kwenye mizani ya Qur’an na utakapoona kuwa haikubaliani na Qur’an, basi itupilie mbali. Sasa ndugu Nasser Amour, kweli hadithi kama hii itaweza kukubaliana na Qur’an? Jibu, haikubaliani na Qur’an, na kama ni hivi, ilikuwaje ikanukuliwa na kusomeshwa watu? Hivyo ndugu Nasser, Imani hii haipo kabisa kwa Mashia

 

 

 

Hashim Mon 11/03/02 02:32            Re: [zanzinet] Ni kweli Shia wanaamini hivi?            

Assalaam Aleykum

Ndugu M. Faraj, mimi naelewa vizuri sana kama si wewe uloyaleta humu, lakini naelewa vizuri sana ni wewe uloyatayarisha, hivyo majibu yangu yalikuwa yanakwenda kwa ndugu Amour Nasser ambae yeye ndie alieuliza hili suala japo kuwa mimi katika ile barua yangu nimekutaja lakini ilikuwa haimaanishi ni wewe uloleta.

Pia umesema kuwa hutopendelea kuuendeleza huu mjadala, hivyo ni sawa, kwani hata kwa upnde wangu naona ni hivyo kwasababu mimi na wewe tunaelewa vizuri sana nini natija yake itakuwa. Ni kweli kabisa ukumbi wa majadilianio ya kimadhehebu umefunguliwa rasmi lakini ni nani alopeleka masuala au majadiliano tokeya hapo mwanzo ulipofunguliwa?

Kuhusu kitabu kinachoitwa Al-Kafi mara nyingi sana watu washeeleza vya kutosha mpaka wewe binafsi yako ukaelezwa ya kuwa udhaifu wa hadithi zilizomo ndani ya vitabu vya kishia ni kuzipima na mizan, ilivyo wewe ni mtu wa elimu ya kiasi chako natumai unaelewa nini nimekusudia upimaji wa hadithi, zaidi yeye mwenye al=kuleyni amezungumzia kuhusu suala hili pia na hii naamini unaelewa vizuri sana..

Hadithi inaweza kujulikana kama ni dhaifu pale unapoiona inapingana na Qur'an. Juu ya yote hayo ikiwa Al-Kuleyni mwenyewe keshasema hadithi zake zichunguzwe kwa kupitia kwenye mizan ya Qur'an, sasa zaidi lipi unataka?

Katika barua yangu ya mwanzo nimeeleza wazi kuwa kitabu cha Al-Kafi ni kitabu kizito kwa Mashia, pia nikasema kuwa juu ya uzito wake hakuna Alim yoyote yule alothubutu kusema kuwa hadithi zote za al-Kafi ni sahih. Hawo Maulumaa ulowasoma wewe na kusema kuwa wanasema kitabu cha al-Kafi ni kitabu kikubwa kwa Mashia, kwa hilo halikataliki, lakini hakuna Alim aliekubali kitabu cha al-Kafi chote ni sahih.

Katika barua yako umesema:

Nne, kama hadithi hizo ni za uongo kama unavyosema, basi mbona wanaendela kupiga chapa tu vitabu hivyo kila siku tena bila kuwajulisha watu juu ya uongo uliomo ndani yake. Maana unapofungua kitabu na kusoma hadithi hizo huoni mahali popote panapoandikwa kuwa hadithi hizo ni dhaifu, basi sijuwi wewe mwenzangu umefanya wapi tahakiki hiyo?

Kuendelea kuchapishwa hadithi za Al-Kafi sio thibitisho kuwa hadithi hizo ni sahih kama unavyoelewa wewe. Kila chapa ya al-Kafi utaziona hadithi hizo hizo zimo ndani, leo zikajatolewa hizo dhaifu, kesho wewe utakuja nukuu hadithi iliyomo ndani ya al-Kafi na kusema kuwa hadithi hii sasa huipati katika chapa mpya lakini utaipata chapa ya mwaka fulani na huenda ukaendelea kusema kuwa "Unaona hawa Mashia walivyo? Eti sasa wameitowa hadithi hii lakini chapa ya mwaka fulani imo", hii ndio sababu mojawapo hazitolewi hizo hadithi dhaifu. Jee, unaelewa kuwa kuna Lujna imeundwa huko Saudia ya kuipitiya Bukhari na Muslim?

Ukaendelea kusema kuwa:

Ndugu Hashim kumbuka kuwa mlileta hadithi ya Nabii Musa (AS) na namna Mwenyezi Mungu alivyojaalia jiwe liondoke baada ya kuweka nguo zake juu yake mkatuambia kuwa sisi tunafuata hadithi za uongo – lakini tulipojaaliwa kupiga mbizi ndani ya vitabu vyenu na kuona kuwa na humo pia hatdithi hiyo imeandikwa mkasema maneno haya haya kuwa vitabu vyetu ni vya uongo.

Mambo ya Nabii Mussa hapa sio pahala pake, hata hivyo umeyaleta mimi nitasema machache tu.

Hadithi hiyo ikiwa inapatikana katika vitabu vya kishia, ndio ina usahih gani? Hapa ndipo khasaa pa kufahamu msimao wa Mashia juu ya hadithi, ikiwa khadithi hii inapatikana katika kitabu cha Kishia na bado Mashia wakakamata kamba ile ile ya kusema ni dhaifu, sasaa wewe unapata shida gani pale wanaposema kuwa hadithi sio sahih? Ni hapa pakuweza kuelewa msimamo wao juu ya hadithi zilizomo ndani ya vitabu vyao au vya kisunni.

Mwisho kabisa ningelikuomba kitu kimoja nacho ni muhimu sanaa kuliko maudhui hii tunayoyazungumza. Siku zote unapoleta malalamiko yako, usijaribu kuchanganya mambo hayajazungumzwa, kwa mfano wa haya maneno yako "

Leo mnatuambia sisi pagans tunaamini kuwa Nabii Issa alipaishwa mbinguni, kesho mnatuambia kuwa sisi ni wapotofu tunawafuata Abubakar na Omar mara mnatuambia kuwa Imam Bukhari na Muslim ni waongo.

Shekhe, huu si uadilifu kabisa. Mimi sikutegemea mtu kama wewe na hasa kwa cheo chako ulichonacho kuwa utasema maneno kama haya. Jee, unajuwa kipande chako cha haya maneno yanaweza kusababisha mzozo humu? Ni afadhali sana kuyanuku maneno yalivyoandikwa kuliko kutowa ndani ya kichwa chako, na kama kuna mjumbe yoyote alokwita wewe pagan basi ni afadhaali umrudie yeye sio "mimi" wala sio "nyinyi". Maisha yote usitumie neno "sisi, nyinyi au wale" mpoint yule mtu alosema na uyanukuu maneno yake kama alivyoandika.

Ahsanteni

Nduguyo

Hashim

 

 

Muhammad Aly       Mon 11/03/02 16:36            Re:[zanzinet] Ni kweli Shiaa wanaamini hivi? / ombi muhimu 

 

 

 

Assalam alaykum,

 

Wananeti/ Kamati ya Nidhamu/Bwana Nidhamu

 

Nilidhani umesikia nasaha za bwana Idrisa A. Rai, na kwamba katika wavu huu

hamtakuwa tena na bugdha za kimadhehebu. Mimi naona kuwa watu kama nyinyi

hamuwezi kukaa bila ya kuandika mambo haya ya kuwabugudhi wenzenu kwa maana

hamuoni raha katika nyoyo zetu isipokuwa kwa kuandika ya kuleta mfarakano

baina ya waislamu.

 

Ukumbi wa haya umewekwa ni kwa sababu gani wewe na wenzako hamjataka kuja

huko kijiweni????

 

La kama unataka jawabu rasmi ya haya unayoyaandika, naiomba Kamati ya

Nidhamu iniruhusu nikujibu, natowa ombi langu hili nipewe jawabu kabla ya

siku tatu kupita na kama hamkunipa jawabu ya kuruhusiwa au kutoruhusiwa mimi

nitajibu na sitaki bugdha pale nitakapoanza kukujibu.

 

Nawaomba msije mkaniambia kuwa nawatukana au nimeleta mfarakano katika wavu,

hivyo kama mnaona kuwa kuna maslahi kwa Ukumbi huu kujibiwa kwa kirefu na

kwa dalili sahihi makala za Bwana Nasser Amour naomba mniruhusu kwa barua

rasmi.

 

Ahsanteni, ndugu yenu Muhammad Aly

 

 

Muhammad Aly       Mon 11/03/02 16:40            Re: [Zanzinet] SHIA V/S SUNNI / msiba mkubwa huu!! 

 

 

Naam, tuechoka na haya, lakini hawa akina nasser amour na huyo aliyeanza

kuleta sites zake na mawahabi wenzao wameyaleta haya ili kuleta huo

mfarakano wa waisilamu, wao wanapata faida kubwa. Wanatabaruku na damu

inayomwagika baina ya waisilamu, wanapata pepo kwa kuwatukana mashia na

masunni ambao wanawaita ahlilbid'aa kama hao waisilamu wa dhehebu la

Kishafi, Kihanafi na Kimaliki!

 

Sisi nia yetu ni kuelimishana na sio kubugudhiana kwa kutumia madhehebu,

nasaha za Bwana Idrisa A. Rai mimi binafsi niliziunga mkono, lakini wapi,

mawahabi hawasikii, inasikitisha kuona kuwa wengi kati ya wanachama wa

ukumbi huu bado kuelewa kuwa, hawa wanaoleta ugomvi na uhasama baina ya

waisilamu si sunni wala si shia bali ni mawahabi na masalafi ambao nia yao

kubwa ni kuleta tofauti baina ya waisilamu, tofauti ambazo zimeshaliwa na

historia ya ulimwengu...

 

Any way hiyo ndio siasa yao bali kama jambo hili la kubugudhiana kimadhebu

linakubaliwa na Ukumbi huu, mimi binafsi naomba kwa Kamati ya Nidhamu

niruhusiwe kuleta makala za kimadhehebu kwa barua rasmi.

 

Ingawa sipendi hayo na mara nyingi nimesema haya, mnaweze kurejea kwenye

archives mtaona humo nasaha zangu...

 

Maa salaam

 

Ndugu yenu, Muhammad O. Aly

 

 

 

>From: "dost dosteen" <dost600@hotmail.com>

>To: zanzinet@zanzinet.org

>Subject: [Zanzinet] SHIA V/S SUNNI

>Date: Sun, 10 Mar 2002 15:18:20 +0300

>

>

>

>

>SHIA/SUNNI/SHIA/SUNNI/SHIA/SUNNI/SHIA/SUNNI/SHIA/SUNNI/SHIA/SUNNI/SHIA/SUNNI/SHIA/SUNNI/SUNNI/SHIA/SUNNI/SHIA/SUNNI/SHIA/SUNNI/SHIA/SUNNI/SHIA/SUNNI/SHIA/SUNNI/SHIA/SUNNI/SHIA/SUNNI/SHIA/SUNNI/SHAI/SUNNI/SHIA/SUNNI/SHIA/SUNNI/SHIA/SUNNI

>

>  Baada ya muda mfupi wa kusoma hapo juu utajikuta umechoka na maelezo ni

>boring!!! TUMECHOKA NA HAYA !!

>

>

>_________________________________________________________________

>MSN Photos is the easiest way to share and print your photos:

>http://photos.msn.com/support/worldwide.aspx

>

>_______________________________________________

>Zanzinet mailing list

>Zanzinet@zanzinet.org

>http://www.zanzinet.org/mailman/listinfo.cgi/zanzinet