Inasikitisha kuwaona watu wengine khasa Waislamu wenzetu, kutokana na ujahili wao kufanya maskhara kwa wale wenye kushika siku ya Ashura. Ujahili wao kutokana na uchache wa elimu waliyo nayo, hawajuwi nini wanasema. Mushkila wanayosoma au wanayosikia inasababisha kugusia hisia zao na inawafanya kuwa katika hali ya incitement. Hiyo waliyoyasoma au kusikia wanayakubali bila kuhakikisha yakuwa ni ya kweli au ya uwongo, wanaanza kuwashambuliya wengine. Ingekuwa wanafahamu Quran vizuri na inaingia ndani kabisa katika nyoyo zao, kisha kuifuata hii taalimu yake wangekuwa vingine.
Wataona kitu cha kushangaza kuona mtu anajipiga mwenyewe au kumlilia mwingine. Bila shaka wataona kitu cha kushangaza kwasababu walivyolelewa inaenda kinyume na Ashura. Tuchukuwe mfano wa Kristo wakati atapomuona MUISLAMU ANAPOHIJI, yeye ataanza kucheka na KUONA HAYO MAMBO YA UPUZI. Anaona yakua mtu anazunguka kwenye nyumba ambae MAWE TUPU HAINA CHOCHOTE, KUENDA NA KUREJEA KWENYE JABALI MOJA MPAKA YA PILI (SAFA WA MARWA), kisha kuenda KUPIGA KOKOTE KWENYE UKUTA (JAMARA) HAINA CHOCHOTE. Haitoshi hayo yote tena kuchinja mbuzi au kondo kwa makumbusho ya nabii Ismail (a.s) AMBAE AMEFARIKI ZAMANI KABISA! Kwako wewe Muislamu utaona ni kitu Farzi lakini aliyekuwa amelelewa vingine kwa Ukristo utaona ni kitu ya upuzi. Daima mtu yeyote alivyoleleka huona yakwake ndio sawa na ya mwingine inayo makosa. BINAADAMU ANAPASWA KUWEKA ALIVYOLELEKA PEMBENI NA KUTAFUTA UKWELI, KWA BAHATI MBAYA WENGI WETU HUFUATA WAZEE WAO. Basi hivyo hivyo ikiwa ndugu zetu wa Kisunni wakitaka kujuwa kwanini tunajipiga, kujiumiza na kumlilia Imam Hussain (a.s) kwanza waeke ile ulezi wao pembeni, kisha watafute Ukweli.
Tutalezea mambo mawili ya kujipiga na kujiumiza mwenye.Kwanza tuanze na kujipiga jee inaruhusiwa katika Islam kufanya kitu kama hiyo?
(I) KUJIPIGA MWENYE
Kuhus mambo ya kujipiga tutatizama kwa upande tatu tafauti, kwenye Quran, hadith na watu kwa jumla.
A) Quran Tukufu
Kwenye Quran tukufu kwenye Sura ya ADH-DHAARIYAAT tutamuona SARAH ANAJIPA USONI, wakati alipoambiwa atapata mtoto.
29. Ndipo mkewe akawaelekea, na huku anasema na akijipiga usoni kwa mastaajabu, na kusema: Mimi ni kikongwe na tasa! * 51:29
Ingekuwa kujipiga Usoni ni kitu yenye kukatazwa hapa tungeona aya yenye kupinga hiyo aliyofanya Sarah, Lakini ALLAH HAKUSEMA HIYO WALA HAKUKATAZA.
B) Hadith
1) Mbedu Mwenye kujipiga Kifua na kuwa na msiba
Tutaona kwenye kitabu ya Muwatta ya Imam Malik, yakuwa alikuja mbeduu moja kwa Mtume Mtukufu (s.a.w) na huku AKIJIPIGA KIFUWA NA KUTOWA NYEWELE ZAKE MBELE YA MTUME (S.A.W), kwa sababu amelelala na mkewe wake huku amefunga siku ya Ramadhani, mbele ya Mtume.
Malik's Muwatta
Book 18, Number 18.9.29:
Yahya related to me from Malik from Ata ibn Abdullah al-Khurasani that Said ibn al-Musayyab said, "A bedouin came to the Messenger of Allah, may Allah bless him and grant him peace, beating his breast and tearing out his hair and saying, 'I am destroyed.' The Messenger of Allah, may Allah bless him and grant him peace, said, 'Why is that?', and he said, 'I had intercourse with my wife while fasting in Ramadan.' The Messenger of Allah, may Allah bless him and grant him peace, asked him, 'Are you able to free a slave?', and the man said, 'No.' Then he asked him, 'Are you able to give away a camel?', and the man replied, 'No.' He said, 'Sit own,' and someone brought a large basket of dates to the Messenger of Allah, may Allah bless him and grant him peace, and he said to the man, 'Take this and give it away as sadaqa.' The man said, 'There is no one more needy than me,' and (the Messenger of Allah, may Allah bless him and grant him peace), said, 'Eat them, and fast one day for the day when you had intercourse.' "
Katika hii kisa tunaweza kufikiria ukweli kama ifuatao :-
a) Mbedu Muislamu alikuwa ni Sahabi wa Mtume (s.a.w).
b) Yeye alikuwa akijipiga kifuwa na kutowa nywele zake mbele ya Mtume (s.a.w) ambae hakuikataza jambo hilo wala kumkataza yeye kwa kufanya hivo.
c) Hivyo alivofanya mbedu kutokana na maumivu ya roho aliyoipata kwa kuvunja Saumu yake.
d) Kisa hichi imenukuliwa katika Hadith Sahih katika Kitabu ya Masunni.
Msiba ya Karbala ni zaidi yenye kusikitisha na kuumiza kuliko ya kuvunja Saumu . Kutokana na hiyo, vipi itakuwa kujipiga kifuwa kukatazwa?
2) Kujipiga kwa Bilal na kushika Msiba
Sheikh Abdul Haq Mohaddis Hanafi Dehlavi ambae anatambuliwa kuwa moja wa wakubwa wa Maulama wa kimadhehebu ya Sunni, ameelezea kadhiya katika ugonjwa kali ya Mtume (s.a.w), katika kitabu chake inayoitwa ‘Modaarejun Nubuwwat’ juz II uk 544 yakuwa :
“Bilal amejitokeza kwa kujipiga kichwani na hukuwa akilia kwa makele (katika chumba cha Aisha)”
Hata katika kadhia hii hamna Sahaba yeyote mwenye kulalamika au kumkataza aliyokuwa akifanya Bilal, khasa Muazzin wa Mtume (s.a.w). Zaid ya hivyo, Mtume (s.a.w) bado alikuwa hai na hajafariki. Hii ilikuwa masikitiko kubwa. Vipi tena anavyo fanyiwa kama hivyo Imam Hussain (a.s) (kama alivyo fanya Blila) huwa katika kadhiya inayokatazwa?
3) Kujipiga kwa Aisha na kushika Msiba
Katika Musnad ya Imam Hanbal juz 6, uk 274; Aisha alikuwa akilia kwaajili ya mauti ya Mtuku Mtume (s.a.w) pamoja na wanawake wengine kwa kujipiga vichwa vyao.
4) Kujipiga kwa Fatima Zahra na kushika Msiba
Tena katika hiyo hiyo kitabu inayoitwa ‘Modaarejun Nubuwwat’ juz 2, uk 163 ya Alim mkubwa wa Kisunni, Sheikh Abdul Haq Mohaddis Hanafi Dehlavi ameelezea yakuwa wakati Fatima Zahra (a.s) aliposikia mvumo yakuwa Mtume (s.a.w) amekukwa Shahid katika Uhud, ametoka nje ya nyumba yake kwa kukimbiya na huku akijipiga kichwani.
Jee hii haidhihiri kutokana na kujipiga kichwani katika hali ya huzuni kwaajili ya Shahid ni vile vile inakubaliwa katika dini, kwa sababu Fatima (a.s) alikuwa mwenye kujuwa sana kanunu za kidini na hivyo hivyo ni si mtu mwenye kufanya makosa kama katika aya tat-hir (33:33).
5) Wenye Kujipiga vifuwa na Kushika Msiba kwaajili ya Mauti ya Imam Ahmad bin Hambal
Katika kitabu kinachoitwa ‘Hayatul Aaiwan’ imeandikwa hivi:
“Khalifa Mutawakkil ameamrisha yakuwa katika mahali anaposaliwa maiti ya Imam Ahmad bin Hambal (moja katika aliyoanzisha Madhehebu ya Kisunni) WATU WAJIPIGE VIFUWA. Kutokana na riwayat yakuwa kiasi ya watu 25,000 pamoja na Waislamum Mayahudi, Makristo na Majusi wamekusanyika and kumsikitikiya Ahmad bin Hambal kwa KUJIPIGA VIFUWA.”
Upate kujuwa yakuwa huyu Khalifa Mutawakkil ni yule yule ambae ameivunja kaburi ya Imam Hussain (a.s) kwa ukamilifu. Baada ya hivyo alikuwa anayo mapenzi kubwa kwa Imam Ahmad Hambal, yakuwa SIO PEKE YAKE ALIJIPIGA KIFUWA, LAKINI AKAMRISHA HATA DINI ZINGINE WAFUATE MFANO WAKE.
6) Wenye kumlilia Yesu wajipiga vifuwa
Tukitzama hata enzi hiyo ya zamani ilikuwa kawaida kumlilia mtu kwa kujipiga vifuwa. Hata katika enzi ya hiyo Yesu wakati aliposulibiwa, waliyokuja kutizama hivyo anavosulibiwa na kuona yakuwa amefariki, wakashika msiba na kujipa vifuwa.
Luke 23:46-48
46 And when Jesus had cried with a loud voice, he said, Father, into thy hands I commend my spirit: and having said thus, he gave up the ghost.
47 Now when the centurion saw what was done, he glorified God, saying, Certainly this was a righteous man.
48 And all the people that came together to that sight, beholding the things which were done, smote their breasts, and returned.
(KJV)
C) Kawaida ya Watu hujipiga wenyewe
Binaadamu gani katika maisha yake ataweza kujidai yakuwa yeye hakuwahi kabisa na hatojipiga kwa mwenyewe! Ikiwa atajaribu kujidai namna hivyo basi atakuwa anajidanganya mwenyewe. Sisi binaadamu tumeumbika kujipiga wenyewe wakati chochote yenye kutufurahisha au kutuhuzunisha.
Tunakwenda kwenye mikutano, party na manasiba zingine, wakati unapofika kumshangiliya mtu kwa aliyoifanya tunaanza kupiga makofi. Wengine watajipiga kwa nguvu hata mikono zao zitakuwa nyekundu, hapa hamna mtu kulalamika na kusema eti TUNAJIUMIZA WENYEWE!!! Sio yakuwa hamna mtu wa kulalamika lakini SOTE TUNAUNGANA PAMOJA KWA KUPIGA MAKOFI!!
Hivyo hivyo tunaposikia habari ya kustaajabisha au ya huzuni tunajipiga vichwani, kwenye vifua au mahali popote kwenye mwili wetu. Utaweza kuwaona hii tabia kwa binaadamu wote, haichaguwi yakuwa yeye ni Sunni, Shia, Mkristo, Myahudi au yeyote yule. Tena HATUSIKI MALALAMIKO KWA WALE WENYE KUWALAAMU MASHIA, ETI WANAJIPIGA KWAAJILI YA IMAM HUSSAIN (A.S)!!! Chukuwa mfano kwenye Biblia utaona hayo mamboa :
Luke 18:13
13 And the publican, standing afar off, would not lift up so much as his eyes unto heaven, but smote upon his breast, saying, God be merciful to me a sinner. (KJV)
Ajabu hii Dunia kwa wale wenye KUFUATA WALIVYOLELEWA BILA KUTAFUTA UKWELI!!!
(II) KUJIUMIZA MWENYE
1) Mbeduu kuchana chana nyewele zake
Tumeona kabla vipi Mbedu alipokuja kwa Mtume (s.a.w) na huku akitowa nyewele zake, jee hii sio kitu cha kujiumiza mwenye, mbona hapa Mtume (s.a.w) hakuikataza jambo hilo wala kumkataza yule mwenye kufanya hivo.
2) Kujiumiza mwenyewe Sahaba Uwais Qarni
Takriban Waislamu wote wanamjuwa Sahabi Owais Qarni (r.a), ambae amesifiwa upande wote, upande wa Shia na Maulama wa Kisunni. Alikuwa akimpenda sana Mtume Muhamamd (s.a.w). Wakatai habari ilipomfika Yemen yakuwa meno mbili za Mtume (s.a.w) yamevunjika katika vita ya Uhud, yeye akangowa meno zake zote. Wakati Mtume (s.a.w) alipopata habari Medina yakuwa Owais amengowa meno zake zote, Mtume (s.a.w) kwa kustaajabu na sauti kubwa akasema : “Kweli Owais NI RAKIFIKI KHASA.” Kisa hii utapata katika kitabu inayoitwa ‘Tazkeratul Aulia’ ya Sheikh Fariddun Attar, hivyo hivyo kwenye kitabu ingine inaitwa ‘Ihsanul Uyun’ umaarufu wake inajulikana kwa jina la ‘Seerate Halbia’ Juz II, Uk 295.
Hapa tutatambuwa yakuwa kungowa jino moja ni maumivu yake zaidi mara elfu kuliko kwa kujipiga kwenye kifuwa kwa muda masaa ngapi. Tutaweza kuongeza yakuwa maumivu ni zaidi kuliko kwa kujipiga kwa minyororo au visu (zanjir), kwa sababu wale wenye kujuwa vipi ipo maumivu yakutowa jino na vipi imempa maumivu Owais Qarni kwa kungowa meno zake zote. Kwa ukweli ilikuwa ushujaa kubwa kwa kufanya naman hivyo.
Kwa wale wenye kupinga kwa kushika msiba wa Imam Hussain (a.s), na kwa wote Mashuhadaa wa Karbala, kawaida wanauliza suala yakuwa jee Mtume Muhammad (s.a.w) ametowa amri kushika hii msiba ya Imam Hussain (a.s)? Jawabu ya suala yao ni hii : Jee Mtume Mtukufu (s.a.w) amemwamrisha Owais Qarni kwa kutowa meno zake? Jee amewamwarisha yule Mbedu ajipige kufuwa? Je amewaamrisha kina Bilal na Aisha kwa kujipiga vichwa vyao? Hivyo hivyo Mtume (s.a.w) hakumwamrisha Fatima (a.s) wakati alipokuwa akijipiga kichwani aliposikuwa mvumo yakuwa Mtume (s.a.w) amekuwa Shahid katika Uhud. Sababu yakutokuwa amri kutokana na ushikaji wa msiba au kukataza ni wazi kabisa, hii yote kutokana na mapenzi na huzuni kwa Mtume (s.a.w) ndio maana hakukatazwa kabisa. Hivyo hivyo wazi kabisa kwa kushika msiba ya Imam Hussain (a.s) kwa kujipiga vifuwa au Zanjir hii ni kutaka kuonesha kwa mwili (Physical Expression) kwa mapenzi na maumivu ambae iliyomfikia Imam Hussain (a.s) na haioneshi chochote isipokuwa MAPENZI NA IMANI.